DEREVA DARAJA II

Website Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

DEREVA DARAJA II

Taasis: Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

Idadi ya Nafasi: 4

Muda wa Maombi: 15/09/2025 – 28/09/2025

Majukumu ya Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

Sifa za Mwombaji

  • Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
  • Awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Malipo

TGS B

To apply for this job please visit portal.ajira.go.tz.