
Website Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
DEREVA DARAJA II
Taasis: Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Idadi ya Nafasi: 4
Muda wa Maombi: 15/09/2025 – 28/09/2025
Majukumu ya Kazi
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Malipo
TGS B
To apply for this job please visit portal.ajira.go.tz.